Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo Taasisi za Serikali, Sekta binafsi, Wafanyabiasha pamoja na Wananchi kuchangia harambee ya ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya ambao utagharimu Shillingi bilioni 5.8.
Akizungumza leo tarehe 25/5/2023 Mkoani Mbeya katika uzinduzi wa harambee iliyokwenda pamoja na matembezi, Mhe. Homera amesema kuwa kila mmoja anapaswa kuchangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa hosteli kutokana wanafunzi wa kike wanasoma katika mazingira sio rafiki.
"Vijana wetu wa kike wanakaa mtaani ambapo kuna changamoto nyingi ambazo zinawafanya wasifanye vizuri katika masomo yao, kuna vishawishi kama hawajawa makini wanaweza kupata maradhi kutokana na mazingira wanayoishi" amesema Mhe. Homera.
Mhe. Homera amesema wananchi wa Mkoa wa Mbeya kupitia Rasi wa Ndaki ya Mbeya tayari wameanza safari ya kwenda kujenga hosteli za watoto wa kike ili kuhakikisha wanasoma katika mazingira rafiki.
"Nawapongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuja na wazo hili, mimi Mkuu wa Mkoa siweze kuwaacha nitahakikisha hosteli zinakamilika na watoto wa kike watapata hosteli za kisasa na kuishi katika mazingira mazuri" amesema Rc Homera.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, amesema lengo ni kuchangisha fedha kwa ajili ujenzi hosteli na kuwasaidia wanafunzi ili kuepukana na changamoto katika masomo yao.
Prof . Mwegoha amefafanua kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani ambazo ameweka mwenyewe ili kuhakikisha miundombinu ya elimu inaimalika nchini.
Ili kufikia lengo kwa wakati viongozi wa serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi kwa ujumla wanapaswa kushiriki harambee ya ujenzi wa hosteli kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kupitia control namba 994180331310.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera akiwa katika matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wakike
wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya. Matembezi hayo yalianzia Kituo cha Basi cha Kabwe jijini mbeya
hadi viwanja vya ndaki hiyo eneo la Forest leo Mei 25, 2023.
Washiriki wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa kike Ndaki ya Mbeya, Chuo Kikuu Mzumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,
Mheshimiwa Juma Homera wakati akihutumia katika harambee ya kuchangia Ujenzi wa hosteli katika ndaki hiyo leo Mei 25, 2023.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera akichangia harambee ya ujenzi wa Hosteli ya wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya
Mbeya jijini humo leo Mei 25,2023. Pia amewaelezea washiriki wa hatua za kulipia za kuchangia ujenzi kwa kumtumia namba ya malipo 994180331310
alipotembelea eneo zitakapo jengwa hostel hizo chuoni hapo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa William Mwegoha akitoa taarifa ya chuo na kuelezea umuhimu wa harambee ya ujenzi
wa Hostel ya wanafunzi wakike katika Ndaki ya Mbeya leo Mei 25, 2023.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu Shahada ya Kwanza ya Menejimenti ya Rasilimali Watu, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya, Neema Alex
akielezee changamoto alizopitia alipokuwa akikaa nje ya Chuo na umuhimu wa ujenzi wa hosteli hizo katika haramee ya ujenzi wa Hosteli za
wanafunzi wa kike Chuoni hapo leo Mei 25, 2023.
Mwanafunzi wa darasa la Tano, Shule ya Msingi Ndola Mbalizi Abubakari Shabani Mwamba akichangia shilingi 400 katika harambee ya ujenzi wa hosteli za
Kike Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Mbeya. Na kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Mbeya na vitongoji vyake kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.
Juma Homera kwenye harambee hiyo.
Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,(Taaluma Utafiti na Ushauri) Dkt Eliza Mwakasangula akitoa neno la shukrani kwa niaba ya
Menejimenti na wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa Harambee ya
kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike.