MAKAMU MKUU WA CHUO NA MENEJIMENTI WATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA CHUO KIKUU MZUMBE NDAKI YA MBEYA

Makamu mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amewaongoza wajumbe wa Menejimenti kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Ndaki ya Mbeya.
Miradi iliyokaguliwa na kutembelewa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa jengo la zahanati ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75%, mradi wa ukarabati wa viwanja vya michezo hasa mchezo wa kikapu ambao pia umefikia asilimia 60% na mradi wa ukarabati wa jengo la Hosteli ya Borito.
 
Akitoa ufafanuzi Mhandisi Ndipie Tilon amesema utekelezaji wa miradi hiyo iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji na kuwahakikishia wajumbe wa Menejimenti pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo kwamba miradi hiyo itakamilika kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora vilivyokubalika kwa mujibu wa mkataba.
"Kwa sasa tupo hatua za mwisho kukamilisha miradi hii, hivyo niwahakikishie Menejimenti na Makamu Mkuu wa Chuo kazi inakwenda kukamilika hivi karibuni" amesisitiza Mhandisi Ndipie.
Prof. Mwegoha pamoja na Menejimenti wamemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa miradi hii inakamilika kwa wakati kama walivyo kubaliana.
 
 Kwa taarifa zaidi na picha za takio hili, Bofya Hapa

 

Address

MBEYA CAMPUS COLLEGE
Forest Area - Mbeya City
Mzumbe University
P.O.Box  6559, Mbeya, Tanzania
Tel: +255 (0) 252502863 /57/58
Fax: +255 (0) 252502862
email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.